Papa Tawadros II aapishwa rasmi

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 14:09 GMT
Papa Tawadros II,

Papa Tawadros II,

Papa mtakatifu mpya wa Kanisa la Coptic nchini Misri ametawazwa rasmi hii leo mjini Cairo.

Papa Tawadros II, alithibitishwa rasmi kuwa kiongozi mpya wa Wakristu waliowachache, katika sherehe iliyofanyika katika kanisa la St. Mark, mjini Cairo.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 60, anachukua mahala pa Papa Mtakatifu Shenouda III, ambaye aliaga dunia mwezi Machi mwaka huu, baada ya kuliongoza kanisa hilo kwa miongo minne iliyopita.

Kutawazwa kwake kumejiri wakati wakristu nchini humo wakiwa na wasi wasi mwingi kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais Hosni Mubarak mwaka uliopita.

Taifa hilo limeshuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya waumini wa kanisa hilo na pia makanisa kadhaa nchini humo yameshambuliwa tangu kuporomoka kwa utawala wa rais Mubarak.

Raia wengi wana shaka nyingi kuhusiana na kuibuka kwa makundi mengi ya Kiislamu.

Inakadiriwa kuwa Wakristu nchini Misri ni kati ya asilimia 5-10 ya idadi yote nchini humo ambao wengi ni waislamu wa dhehebu la Kusini.

Misri ndilo taifa la pekee katika eneo la Mashariki ya Kati iliyo na idadi kubwa zaidi ya wakristu.

Rais wa nchi hiyo ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu Mohammed Mursi hakuhudhruia sherehe hiyo lakini waziri wake mkuu Hisham Qandil alikuwepo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.