Mlipuko Nairobi wazua fujo

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 19:05 GMT
Mwenye duka wa Eastleigh, Nairobi

Watu kama watano wamekufa katika mlipuko kwenye mtaa wa Eastleigh wa Nairobi wenye wakaazi wengi wa Kisomali.

Shambulio lililenga basi la "matatu" lilokuwa likitoka kati ya mji.

Naibu msemaji wa polisi wa Kenya, Charles Owino, alieleza kuwa bomu liliripuka ndani ya basi lilipokuwa likipita mtaa wa Eastleigh.

Dakika chache baadae vijana waliokuwa na hasira waliwalenga watu wa jamii ya Kisomali kwenye mtaa huo.

Mtu aliyeshuhudia tukio hilo aliiambia BBC kwamba aliona makundi ya Wasomali wakijipanga kupambana na vijana hao ambao walikuwa wakivamia nyumba zao.

Polisi ilibidi kufyatua risasi hewani kuwatawanya watu.

Hili ni shambulio la karibuni kabisa katika miji ya Kenya tangu jeshi la nchi hiyo kuingia Somalia mwaka jana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.