Vurugu zazuka tena mjini Nairobi

Imebadilishwa: 19 Novemba, 2012 - Saa 10:56 GMT

Athari za fujo

Hali ya wasiwasi imetanda katika mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi baada ya mlipuko wa jana jioni.

Polisi wanakabiliana na vijana wanaojaribu kuwashambulia Wasomali kuhusiana na shambulizi hilo la jana la kigaidi lilotokea katika eneo hilo.

Uhasama huu ulizuka baada ya kulipuliwa kwa basi dogo la abiria Eastleigh, lililosababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi zaidi ya wengine 30.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa na polisi zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa kwenye ghasia hizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.