Wapiganaji wa Tuareq watimuliwa

Imebadilishwa: 20 Novemba, 2012 - Saa 13:39 GMT
Wapiganaji wa Tuareq

Wapiganaji wa Tuareq

Wapiganaji wa waasi Kaskazini mwa Mali wanasema wame watimua wapiganaji wa kabila la Tuareg kutoka mji wa jangwani wa Menaka.

Lakini wapiganaji hao wa Tuareq wamekanusha madai hayo, wakisisitiza kuwa mapigano bado yanaendelea.

Wiki iliyopita, viongozi wa muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, waliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi Elfu Tatu, ili kusaidia wanajeshi wa serikali kuukomboa eneo la Kaskazini mwa Mali.

Hapo jana mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni, wa muungano wa ulaya EU waliidhinisha maafisa Mia Mbili Hamsini wa Kijeshi kutumwa nchini humo ili kutoa mafunzo wanajeshi wa nchi hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.