Viongozi wa Maziwa Makuu wajadili DRC

Imebadilishwa: 24 Novemba, 2012 - Saa 12:32 GMT

Viongozi wa nchi 11 za Afrika wanakutana mjini Kampala, Uganda, kujaribu kutafuta suluhu katika vita vya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Mkimbizi wa Goma akiingia kambi ya Umoja wa Mataifa nje ya Goma

Wapiganaji mashariki mwa Congo walisonga mbele zaidi ndani ya ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Alkhamisi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa awali juma hili iliishutumu Rwanda kuwa inawasaidia wapiganaji hao, shutuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.

Kiongozi wa kiraia wa kundi la wapiganaji wa M23 piya yuko kwenye mkutano wa Kampala.

Haijulikani mchango wake ni wa kiasi gani kwenye mkutano huo wa dharura wa viongozi wa kanda ya Maziwa Makuu.

Wapiganaji wanataka kuzungumza ana kwa ana na serikali ya Congo.

Lakini Rais Joseph Kabila anasema atazungumza tu na Rwanda.

Huku nyuma wapiganaji wanaendelea kusonga mbele wakielekea kusini na kaskazini kutoka shina lao mjini Goma.

Umoja wa Mataifa unasema kikosi chake kilioko huko kitajaribu kuwazuwia wapiganaji wasisonge mbele, lakini umesema askari wake wa kuweka amani hawawezi kubeba jukumu la jeshi la serikali ya Congo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.