Majaji wa Misri wamlaumu Rais Morsi

Imebadilishwa: 24 Novemba, 2012 - Saa 16:40 GMT

Majaji wa Misri wamelalamika juu ya uamuzi wa Rais Mohammed Morsi wa kuchukua madaraka zaidi, kuwa hatua hiyo inashambulia uhuru wa majaji hao.

Mahakama ya Misri

Siku ya Alkhamisi Bwana Morsi alisema alichukua hatua hiyo kwa masilahi ya wananchi wote wa Misri, na majaji hawawezi kukaidi madaraka yake mepya.

Majaji katika mji wa Alexandria, kando ya bahari ya Mediterranean, wanasema wanagoma kuonesha mlalamiko yao.

Hapo jana kulifanywa maandamano makubwa sehemu mbali-mbali za nchi kupinga hatua ya rais.

Maandamano mengine yanapangwa kufanywa Jumamosi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.