Moto wa pili kiwandani Bangladesh

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 08:24 GMT

Jamaa za waathiriwa wa mkasa huo watambua maiti

Moto umezuka tena katika jengo la ghorofa lenye viwanda kadhaa vya kutengeneza nguo katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka.

Msemaji wa polisi alisema moto huo uliotokea Jumatatu ulianza katika orofa ya tatu ya jengo lenye orofa 12,kwa mujibu wa shirika la habari la AFP lilisema.

Hakuna habari zaidi kuhusu majeruhi na polisi wanasema kwamba hawajui idadi ya watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo.

Moto huu umezuka siku mbili baada ya kiwanda kingine nje ya Dhaka kuteketea na kuwaua zaidi ya watu 100.

Maelfu ya wafanyakazi kutoka kiwanda cha nguo cha Tazreen waliandamana Jumatatu, wakidai wapewe mazingira bora zaidi ya kazi.

Walisema kwamba watu wengi walikwama ndani ya jengo, katika moto huo uliozuka jioni Jumamosi, na kuongezea kwamba jengo hilo lilikuwa halina milango inayotumika kunapozuka moto.

Hali duni ya usalama

Moto wa Jumatatu ulianza katika kiwanda cha nguo cha Euro-Bangla mnamo 10:05 asubuhi (04:05 GMT), maafisa walisema.

"Unaonekana kama moto mkubwa sana. Makundi ya wazimamoto wameshawasili na wanajitahidi kuuzima," afisaa mmoja wa kuzima moto wa ngazi ya juu aliiambia AFP.

Duru zinasema kwamba takriban watu wanane walijeruhiwa.

Wazimamoto wajitahidi kuzima moto

Kilichoanzisha moto huo hakijajulikana bado.

Mioto inayowaua wengi hutokea mara kwa mara katika viwanda vya nguo chini Bangladesh, ambayo bi biashara kubwa.

Hali duni ya kazi, nyaya mbovu za umeme, na kuweko kwa wafanyikazi wengi kupita kiasi ni chanzo cha mioto kadhaa inayotokea kila mwaka.

Kuna karibu viwanda 4,500 nchini Bangladesh, vinavyowaajiri zaidi ya watu milioni 2.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.