Watoto 10 wauawa chini Syria

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 12:26 GMT

Mabomu ya Cluster ambayo serikali ya Syria imekuwa ikitumia katika mapigano yanayoendelea nchini humo

Wanaharakati nchini Syria wamesema kwamba ndege ya serikali imeangusha bomu kwenye kiwanja wanapochezea watoto na kuwaua watoto 10.

Kanda ya video iliyowekwa katika internet inaonyesha miili ya watoto wakiwa wamelala chini huku mama zao wakiomboleza.

Watoto hao waliuwawa wakati ndege ya aina ya MiG iliporusha bomu kiwanjani katika kijiji cha Deir al-Asafir, mashariki mwa mji wa Damascus, wanaharakati wa upinzani walisema.

Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu. Waasi waliteka sehemu moja ya kambi ya ndege za kijeshi mnamo siku ya Jumapili.

Kanda hiyo ilionyesha kile kilichoonekana kuwa mabomu madogomadogo kiwanjani. Katika kanda moja, miili ya washichana wawili ilionekana barabarani, huku nyingine ikimuonyesha mama aliyekuwa na huzuni mwingi akisimama ndani ya jengo lililoonekana kama zahanati, akiutazama mwili wa mwanawe wa kike.

Mabomu

Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na madai kila kuchao kwamba serikali ya Syria hurusha mabomu aina ya “cluster” huku mapigano yakizidi kupamba moto, ingawaje madai hayo yamekanwa, alsiema Jim Muir, mwandishi wa BBC.

Mabomu aina ya “cluster”, ni mabomu madogomadogo yanayounganishwa ili kutengeneza bomu kubwa.

Wanaharakati walisema kwamba mabomu mawili ya “cluster” yaliangushwa kijijini humo, huku mtu mmoja akiliambia shirika la habari la Reuters kwamba mabomu madogomadogo 70 yalipatikana.

"Wote waliouwawa walikuwa chini ya miaka 15," Abu Kassem, mwanaharakati huko Deir al-Asafir aliiambia Reuters.

Alisema watu 15 people walijeruhiwa katika shambulizi hilo, na kukana kwamba kulikuwa na wanamgambo waasi kijijini humo. Alisema walikuwepo tu viungani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.