Maandamano kumpinga Rais Mursi wa Misri

Imebadilishwa: 27 Novemba, 2012 - Saa 12:01 GMT

Waandamanaji wanaompinga Rais Mursi wakusanyika Tahrir

Wapinzani wa rais wa Misri Mohamed Mursi wanakusanyika katika medani ya Tahrir Square katika siku ya tano.

Wanatoa wito kwake aondoe kipengee kinachomlimbikizia madaraka .

Kumekuwa na makabiliano kando ya medani hiyo na mabomu ya kutoa machozi yamefyatuliwa.

Maandamano ya chama cha Muslim Brotherhood yamesitishwa.

Maandamano haya yanayofanywa na wakereketwa wa mrengo wa kushoto wa chama cha kisoshialisti ni jaribio la upinzani kwa Mursi kukadiria kiwango cha wafuasi wanaoweza kuwaunga mkono.

Kuna hasira miongoni mwa raia wengi kufuatia amri la Rais Mursi, jambo ambalo linatajwa na wakosoaji wake kama linalohatarisha utawala mpya wa Misri.

Idadi ya waandamanaji inatarajiwa kuongezeka baadaye hii leo.

Kundi la Muslim Brotherhood lina umaarufu wa kukusanya idadi kubwa ya waandamanaji.

Lakini hii leo walifutilia mbali maandamano yaliyopangwa kwa ajili ya kuzuia kuzuka kwa rabsha na hata mauaji.

Tangu amri hiyo kutangazwa mwanachama mmjoa wa Muslim Brotherhood ameuawa na wengine kujeruhiwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.