7 kunyongwa Misri kwa kutengeza filamu

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 14:08 GMT

Maandamano yalifanyika kote duniani kupinga Marekani

Mahakama nchini Misri imewapa hukumu ya kunyongwa watu saba walioshukiwa kuitengeza filamu iliyosababisha kero na ghadhabu katika ulimwengu wa kiisilamu mapema mwaka huu.

Hasira dhidi ya filamu hiyo iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed, ilisababisha maandamano dhidi ya Marekani kiasi cha kuteketezwa ubalozi wake nchini Libya.

Washukiwa hao saba walihukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.

Hukumu hizo ziliidhinishwa na Mufti mkuu nchini Misri ambaye pia ni msomi wa dini ya kiisilamu.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa ni nadra kwa Mufti kupinga hukumu kama hizi.

Filamu hiyo iliyokuwa ya hali ya chini mno, ilitengezwa mjini Carlifonia, Marekani na kutolewa kwenye internet mwezi Septemba.

Miongoni mwa wale walioshtakiwa ni mtengezaji wa filamu yenyewe Morris Sadek ambaye ni raia wa Misri.

Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.