M23 waanza kuondoka Goma

Imebadilishwa: 1 Disemba, 2012 - Saa 13:19 GMT

Wapiganaji wa M23 wa mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wameanza kuondoka katika mji wa Goma ambao waliuteka juma lilopita.

Wapiganaji wa M23 Goma

Malori yaliyobeba wapiganaji hao yalionekana yakipita kwenye barabara inayotoka Goma kuelekea mji wa Kibumba, ambako wakitarajiwa kukaa baada ya makubaliano yaliyofikiwa mjini Kampala, Uganda.

Hapo awali Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa amri ya vikwazo kuwekewa makamanda wawili wanashutumiwa kuwaajiri watoto kupigana, na kuwauwa wale wanaoasi kundi hilo.

Makamanda hao ni Baudoin Ngaruye na Innocent Kaina.

Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji hao - shutuma inazokanusha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.