Kenya yaanzisha sheria kali kwa madereva

Imebadilishwa: 1 Disemba, 2012 - Saa 16:59 GMT

Sheria mpya ya Kenya ya kuzuwia madereva kuendesha magari kihatari, inaanza kutekelezwa Jumamosi.

Mwanamke akata bara-bara nchini Kenya

Wakikutikana na makosa madereva watakabili adhabu kali pamoja na kifungo cha maisha.

Madereva wa mabasi ya abiria, yaani matatu, wamekuwa wakigoma tangu Alhamisi mjini Nairobi na kwengineko, kulalamika juu ya sheria hiyo.

Wengi wanasema kuwa hawamudu faini kubwa.

Lakini serikali imeazimia kupunguza vifo mabara-barani.

Mwaka uliopita Wakenya zaidi ya 3,000 wamekufa kwenye ajali za barabarani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.