Abbas apokelewa kama shujaa

Imebadilishwa: 2 Disemba, 2012 - Saa 13:36 GMT

Rais wa Wapalestina, Mahmoud Abbas, aliwaambia wafuasi maelfu katika Ufukwe wa Magharibi "tuna taifa sasa".

Ramallah wakisherehekea kukubaliwa na Umoja wa Mataifa

Amekaribishwa kama shujaa baada ya kufanya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupiga kura kupandisha hadhi ya Wapalestina.

Akiwahutubia wafuasi wake mjini Ramallah, Ufukwe wa Magharibi, Rais Abbas alisema njia ilikuwa ndefu na shinikizo nyingi sana, lakini Wapalestina walisimama kidete na kushinda:

"Tulikwenda New York, tumebeba ujumbe wa uchungu na ndoto ya watu wetu kukabidhi kwa ulimwengu ujumbe wa haki na uhuru.

Ulimwengu umetoa kauli kwa sauti kubwa.

Umesema: ndio liwepo taifa la Palestina.

Haki za Wapalestina, ndio.

Uhuru wa Palestina, naam.

Uhasama, la.

Makaazi ya walowezi, hapana.

Kuikalia Palestina, sivyo"

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.