Makataa kwa waasi wa FARC Colombia

Imebadilishwa: 3 Disemba, 2012 - Saa 07:28 GMT

Waasi wa FARC

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesema kuwa serikali na wanamgambo wa FARC nilazima wafikie makubaliano yao ya kwanza kufikia mwezi Novemba mwaka ujao.

Rais Santos amesema mazungumzo yanayoendelea hivi sasa nchini Cuba yanapaswa kudumu kwa miezi tu na sio miaka.

Awamu ya kwanza ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC ilimalizika nchini Cuba siku ya Alhamisi.

Kwa wakati huo mpatanishi mkuu wa FARC, Ivan Marquez, amesema palikuwa na taswira nzuri, lakini alisisitiza kuwa pande zote zisifanye haraka kufikia makubaliano.

Amesema hakupaswi kuwa na ratiba yoyote. Rais Santos anaonekena kuwa na fikra tofauti.

Hapo jana Jumapili alisema serikali itatoa hakikisho zote ili FARC isitishe matumizi ya silaha na kujiunga na mfumo wa kisiasa.

Lakini Santos alisisitiza hatokubali jaribio lolote la wanamgambo hao kuchelewesha kusita kutumia silaha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.