Rushwa yakithiri katika nchi za kiarabu

Imebadilishwa: 5 Disemba, 2012 - Saa 10:27 GMT

Ripoti ya shirika la Transparency international kuhusu rushwa

Shirika la kimataifa linalopinga rushwa linasema rushwa bado ipo kwa wingi katika nchi zilizozipindua serikali zao katika harakati za mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika katika nchi za kiarabu.

Utafiti wa shirika hilo kuhusu jinsi rushwa inavyopokewa kimataifa na ndani ya sekta za umma, pia umetaja kuwepo matatizo katika nchi zinazoitumia sarafu ya euro zilizoathirika na mzozo wa kiuchumi.

Wakati huu ambapo migogoro ya kiuchumi na kisiasa inakithiri, ndippo mara nyingi kuna matatizo ya kukabiliana na rushwa.

Na ripoti hii inaashiria kuwa nchi za kiarabu na za mashariki ya kati ambazo hivi karibuni zimeshuhudia mapinduzi bado zinakabiliwa na wakati mgumu kulidhibiti tatizo hili.

Kwa jumla rushwa katika nchi zinazoitumia sarafu ya euro ni kidogo kuliko katika eneo la mashariki mwa Ulaya, lakini shirika la Transparency International linasema kutokana na mzozo wa kifedha, serikali zinapaswa kujitahidi kuimarisha taasisi za uma na kuongeza uwajibikaji.

Utafiti huo unajumuisha zaidi ya nchi mia moja na sabini na Uingereza inajaribu kusalia katika nchi ishirini zilizo juu ya orodha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.