Ziara ya kihistoria ya kiongozi wa Hamas, Gaza

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 13:58 GMT

Khaled Meshaal anahisi kuzaliwa upya

Kiongozi wa kisiasa wa kundi la KiPalestina la Hamas, anayeishi uhamishoni Khaled Meshaal, anazuru Ukanda wa Gaza kwa mara ya kwanza .

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Meshaal kukanyaga ardhi ya Palestina katika muda wa miaka arobaine akiifananisha hisa zake kama kuzaliwa upya kwa mara ya tatu.

Meshaal alienda uhamishoni nchini Syria baada ya vita vya siku sita, mwaka wa 1967, lakini akaondoka Januari mwaka huu na kuanza kuishi Qatar.

Alisema kuwa alihisi kuzaliwa upya mara ya pili wakati Israel ilipojaribu kumuua nchini Jordan mwaka 1997 katika njama iliyotibuka, na kisha siku halisi ya kuzaliwa kwake.

Bwana Meshaal hakuwahi kukanyaga katika eneo la Palestina tangu kuondoka Ukingo wa Magharibi mwaka 1967.

Ziara yake inakuja baada ya makubaliano ya amani kuafikiwa na kisha kumaliza vita vya siku kadhaa kati ya Hamas na Palestina mwezi jana.

Hamas imetawala Gaza tangu mwaka 2007.

Bwana Meshaal aliingia Gaza kutoka Misri katika eneo la mpakani la Rafah, akisujudu na kuibusu ardhi kwa furaha aliyokuwa nayo. Maafisa walisema kuwa mkewe aliwasili Alhamisi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema '' nahisi kama nimezaliwa upya kwa mara ya tatu , na ninamuomba mwenyezi Mungu kuwa wakati wa nne nitakapohisi kuzaliwa upya tena , itakuwa wakati ambapo Palestina itakapokuwa nchi huru''

"Daima Gaza imekuwa moyoni mwangu," alisema Meshaal.

Anatarajiwa kuzuru nyumbani kwa mwanzilishi wa kundi la Hamas ,Sheikh Ahmed Yassin, pamoja na makao ya Ahmed Jabari, kamanda wa jeshi aliyeuawa mwezi Aprili na Israel.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.