M23 wawasili Kampala kwa mazungumzo

Imebadilishwa: 8 Disemba, 2012 - Saa 16:35 GMT

Waakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo na wapiganaji wa M23 wanakusanyika mjini Kampala, Uganda, kwa mazungumzo.

Wapiganaji wa M23 wakiondoka Goma

Juma lilopita wapiganaji hao waliondoka kwenye mji wa Goma, lakini walitishia kuuteka tena iwapo madai yao hayatatimizwa.

Rais Joseph Kabila amesema atasikiliza malalamiko yao.

Watu zaidi ya nusu milioni wamekimbia makwao katika ghasia tangu wapiganaji hao walipoasi na kutoka katika jeshi la Congo mwezi wa Aprili.

Waziri wa taifa wa Uganda anayehusika na mashauri ya nchi za nje, Henry Okello Oryem, amesema kuwa mazungumzo hayo yanaweza kuendelea kwa miezi kadha kabla ya kufikia suluhu na maafikiano kutekelezwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.