M23 waanza kuzungumza na serikali ya DRC

Imebadilishwa: 9 Disemba, 2012 - Saa 16:03 GMT

Waakilishi wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wameanza mazungumzo na wapiganaji wa M23 mjini Kampala, Uganda.

Viongozi wa Maziwa Makuu wakikutana Kampala mwezi Februari pamoja na Rais Kabila (kushoto)

Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga, alisema huo ni mwanzo wa majadiliano baina ya pande hizo mbili.

Wapiganaji wa M23 waliondoka mjini Goma, mashariki mwa Congo, siku nane zilizopita, lakini walitishia kurudi iwapo madai yao hayatasikilizwa.

Rais wa Congo, Joseph Kabila, ameahidi kusikiliza malalamiko yao.

Malaki ya watu wamehama makwao katika ghasia tangu wapiganaji hao walipoasi na kutoka katika jeshi la Congo mwezi wa Aprili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.