Morsi abadili msimamo

Imebadilishwa: 9 Disemba, 2012 - Saa 12:30 GMT
Rais Mursi kwenye mkutano

Rais Morsi wa Misri amebatilisha uamuzi wake wa kujilimbikizia madaraka na kuzusha msukosuko wa hivi sasa.

Lakini hakubadilisha tarehe ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo inatarajiwa kufanywa mwisho wa juma lijalo.

Hii ndio ishara ya kwanza kubwa kuwa Rais Morsi amelegeza kamba.

Lakini haitatosha kumaliza msukosuko wa hivi sasa.

Huku rais akizidi kushinikizwa na upinzani na jeshi, mabadiliko hayo yalitangazwa usiku sana kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Kwa kubadilisha amri yake ya kwanza ya kujizidishia madaraka, sasa rais hana kinga kikatiba kwa maamuzi yake yote.

Lakini bado atakuwa na kinga ya kadiri fulani.

Hata hivo rais alikataa kuahirisha kura ya maoni juu ya katiba iliyopangwa kufanywa Juamamosi ijayo.

Msemaji wa upinzani ameeleza hatua ya Rais Morsi kuwa haina maana yoyote.

Kundi jengine limesema hiyo ni mbinu tu ya kisiasa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.