Mji wa Jowhar Somalia wakombolewa

Imebadilishwa: 9 Disemba, 2012 - Saa 13:38 GMT

Nchini Somalia askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika pamoja na wanajeshi wa Somalia wameuteka mji wa Jowhar kutoka wapiganaji wa Kiislamu, al Shabaab.

Askari wa AU Somalia

Mkaazi mmoja alisema wanajeshi hao waliingia bila ya pingamizi.

Kupoteza mji wa Jowhar ni pigo kubwa kwa al-Shabaab.

Mji huo uko kilomita 90 kaskazini ya Mogadishu, kwenye barabara kuu ya Somalia inayounganisha majimbo ya kusini na kati.

Piya uko katikati ya eneo la kilimo kikubwa cha nchi.

Jowhar ilikuwa ikidhibitiwa na al-Shabaab tangu wanajeshi wa Ethiopia walipoondoka Somalia mwaka wa 2009.

Ulikuwa mmoja kati ya miji mikubwa iliyokuwa bado mikononi mwa al-Shabaab.

Tangu mwaka 2011 al-Shabaab imepoteza makambi yake kadha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.