Waziri mkuu wa Mali ajiuzulu

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 07:59 GMT

Waziri mkuu wa Mali Cheikh Modibo Diarra

Waziri Mkuu wa Mali , Cheikh Modibo Diarra, amejiuzulu. Bwana Diarra ametangaza hayo katika runinga ya taifa baada ya wanajeshi walioongoza mapinduzi ya Mali kumkamata nyumbani kwake Bamako.

Msemaji wa Jeshi la Mali ameiambia BBC kuwa, Diarra, alikamatwa alipokuwa akijaribu kutoroka Mali kuelekea ufaransa na amekuwa akihujumu juhudi za kupatikana demokrasia katika taifa hilo

Alisema agizo la kumkamata lilitoka kwa Kapteni Amadou Sanogo, mkuu wa serikali ya kijeshi ambaye alichukua uongozi baada ya kumpindua aliyekuwa rais Amadou Toumani Toure mwezi Machi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.