Upinzani kupinga rasmi matokeo Ghana

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 15:11 GMT

John Mahama alishinda uchaguzi mkuu wa Ghana lakini upinzani unapinga matokeo ya uchaguzi huo.

Upinzani nchini Ghana umethibitisha rasmi kuwa utapinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo siku ya Ijumaa na Jumamosi.

Chama cha upinzani NPP kimesema kuwa kitakwenda mahakamani kupinga uhalali wa Rais John Mahama. Pia kinasema kuwa kitasusia vikao vya bunge.

Mnamo siku ya Jumapili, tume ya uchaguzi ilimtangaza bwana Mahama kama mshindi wa uchaguzi huo kwa kushinda kwa asilimia hamsini na saba.

Ushindi huu ulimtosheleza kuweza kukwepa duru ya pili dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia arobaini na saba ya kura.

Waangalizi kwenye uchaguzi huo wanasema kuwa ulikuwa huru na wa haki.

Ghana imekuwa ikitolewa kama mfano wa nchi iliyokomaa kidemokrasia katika bara la Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.