Mandela atibiwa ugonjwa wa mapafu

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 13:36 GMT

Mzee Nelson Mandela

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela amepatwa tena na ugonjwa wa mapafu na anaendelea vyema na matibabu .

Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94, amekuwa hospitalini mjini Pretoria tangu Jumamosi .

Hii ni taarifa ya uhakika ya kwanza kutolewa kuhusu afya ya kiongozi huyo aliyepinga utawala ubaguzi wa rangi . Bw mandela alitibiwa mapafu miaka 2 iliyopita.

Habari kuwa Mandelela anatibiwa ugonjwa wa mapafu, bila shaka imemaliza wasiwasi wa siku kadhaa kuhusu ukosefu wa taarifa zozote kuhusu afya yake

Wananchi wa Afrika Kusini wanafuatilia kwa maakini taarifa za afya ya Mandela

Msemaji wa rais huyo mstaafu hakueleza kuhusu ikiwa hali ya Mandela ni mbaya sana au itakuwa sawa lakini alisisitiza kuwa anaendelea kupokea matibabu.

Miaka miwili iliyopita, hali kama hii ilijitokeza kuhusu Mandela baada ya kulazwa hospitalini kwa tatizo la kupumua ingawa aliweza kutibiwa vyema.

Mandela pia alipokea matibabu ya kifua kikuu wakati alipokuwa gerezani, katika kisiwa cha Robben na afya yake, inaendelea kuwavutia watu wengi.

Mac Maharaj, msemaji wa rais, alisema kuwa wanajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kufahamisha watu,kuhusu afya yake lakini pia alitaka kutoingilia kazi ya madaktari pamoja na kutaka jamaa za Mandela kuruhusiwa kumzuru bila matatizo tyoyote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.