Wamisri waanza kupigia Katiba kura

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 10:49 GMT

Maandamano hasimu kuhusu kura ya maoni juu ya katiba mpya

Wananchi wa Misri wanaoishi katika nchi za kigeni, wameanza kupigia kura ya maoni rasimu ya katiba ambayo imezua hali ya mvutano nchini Misri.

Upinzani ulikuwa unataka kura ya maoni kuhusu katiba hiyo kufutiliwa mbali.

Baada ya kucheleweshwa kwa siku kadhaa, balozi za Misri kote duniani zimeanza kuwaruhusu wamisri kupigia kura rasimu hiyo ya katiba.

Mzozo huo ulisababisha maandamano hasimu ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi siku ya Jumanne.

Wakati huohuo, mkuu wa jeshi la Misri ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya mapatano leo kati ya pande zote zinazozozana kuhusiana na kura ya maamuzi kuhusu rasimu ya katiba mpya itakayofanyika Jumamosi.

Generali Abd-al-Fattah al-Sisi ataongoza mkutano huo katika uwanja wa michezo wa Cairo.

Jumanne maelfu ya waandamanaji wafuasi na wapinzani wa Morsi waliandamana kila upande ukijipigia debe.

Wapinzani wa Rais Morsi wanamtaka afutilie mbali kura hiyo ya maamuzi kisema kuwa katiba hiyo inakandamiza haki za binadamu lakini wafuasi wake wanataka katiba hiyo wakisema kuwa itazuia mapinduzi kama yaliyotekelezwa dhidi ya mtangulizi wake Hussein Mubarak.

Wananchi watapiga kura kwa awamu mbili mwanzo siku ya Jumamosi tarehe 15 na baadaye mwishoni mwa Disemba

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.