Korea yafanya majaribio ya makombora

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 10:42 GMT
Makombora ya masafa Marefu ya Korea Kusini

Makombora ya masafa Marefu ya Korea Kusini ikibebwa na gari la jeshi la nchi hiyo

Korea Kusini na Japan zimesema kuwa Korea kaskazini imeendelea na mpango wake wa kufanya jaribio la kurusha roketi ya masafa marefu licha ya kuonywa na jamii ya kimataifa.

Japan imesema kuwa inaokana roketi hiyo ilipitia katika kisiwa chake cha Okinawa.

Msemaji wa serikali ya Japan amesema serikali yake haitavumilia hali hiyo na ameishutumu serikali ya Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio hayo.

Rais wa Korea Kaskazini, Lee Myung-bak ameandaa mkutano wa dharura wa usalama, kufuatua hatua hiyo ya Korea Kusini.

Korea Kaskazini ilikuwa imesisitiza kuwa uzinduzi wa roketi hiyo ni mpango wa shughuli ya amani ya kuweka mtambo wa setlite angani.

Marekani na washiriki wake inasema kuwa majaribio hayo ya zana za nuclear ni ukiukaji wa maazimio ya Umoja wa mataifa.

Jaribo la kwanza la Korea Kusini ambalo lilifanywa mwezi Aprili mwaka huu halikufaulu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.