Mali yapata Waziri Mkuu mpya

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 10:38 GMT
Cheick Modibo Diarra

Waziri mkuu wa zamani wa Mali Cheick Modibo Diarra

Mataifa mbalimbali duniani yameghadhabishwa na jeshi la Mali kwa kumkamata na kumlazimisha waziri Mkuu wa nchi hiyo Cheick Modibo Diarra kujiuzulu.

Marekani imesema kukamtwa kwa bwana Bofya Cheick Modibo Diarra ni pigo kwa utawala wa kidemokrasi nchini Mali.

Kadhalika Umoja wa Mataifa umeitishia kuiwekea Mali vikwazo nayo serikali ya Ufaransa iimesema kuwa panahitajika jeshi ambalo litakaloleta uthabiti katika taifa hilo.

Rais wa Mali sasa amemteua Django Sissoko kuwa waziri Mku mpya.

Tofauti na Jeshi, Bwana Diarra alikuwa amependekeza kuhusisha jeshi la Afrika Magharibi ili kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wanaodhibiti sehemu ya kaskazini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.