Upinzani kupiga kura ya 'hapana' Misri

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 14:32 GMT

Waandamanaji wanaompinga Rais Mohammed Morsi nchini Misri

Upinzani nchini Misri umewataka wafuasi wake kupigia kura ya hapana rasimu ya katiba mpya katika kura ya maoni ambayo imezua utata mkubwa.

Awali upinzani uliwataka wafuasi wake kuisusia kura ya maoni ikisema kuwa katiba mpya inawanyima watu faida za mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika nchini humo na kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.

Wamisri walio ugenini wameanza kuipigia kura katiba hiyo mpya baada ya balozi za nchi hiyo ugenini kuanza rasmi shughuli hiyo.

Lakini Hamdeen Sabahi, mmoja wa viongozi wa upinzani, alisema kuwa watashiriki tu katika kura ya maoni ikiwa majaji pamoja na waangalizi wa kimataifa watakubali kuendesha mchakato huo.

Polisi wakiweka vizuizi barabarani mjini Cairo

Mazungumzo ya kupatanisha pande zinazovutana kuhusu katiba mpya, ambayo yalipaswa kuandaliwa leo, yaliakhirishwa.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa serikali inatuma ujumbe unaogongana kuhusu siku ambayo upigaji kura utakamilika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.