Ushahidi mpya kuhusu kifo cha Samora Machel

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 12:58 GMT

Ramani ya Mozambique

Polisi nchini Afrika Kusini, wameanzisha uchunguzi katika ajali ya ndege ya mwaka 1996, iliyomuua aliyekuwa rais wa Msumbiji, Samora Machel.

Gazeti moja la nchini humo,Times Live, limeandika kuwa ushahidi mpya umejitokeza ndio maana uchunguzi utaanzishwa.

Limesema kuwa ushahidi huo umehusisha maafisa wa usalama wa enzi ya ubaguzi wa rangi.

Ajali hiyo ilitokea ndani ya Afrika Kusini na mara ya kwanza rubani wa ndege hiyo walilaumiwa kwa kutojali lakini ilishukiwa kuwa serikali ya wakati huo ilihusika na ajali hiyo.

Bwana Machel aliyeuawa pamoja na abiria wengine thelathini alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.