Upinzani Syria watambuliwa na Marekani

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 11:16 GMT

Hali nchini Syria ni ya kusikitisha

Urusi imetuhumu vikali hatua ya Marekani kutambua muungano wa vyama vya upinzani nchini Syria kama waakilishi pekee wa halali wa watu wa Syria.

Waziri mkuu wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema kuwa Marekani inakwenda kinyume na juhudi za kufanya harakati za mpito kwa amani na badala yake inataka upinzani kushinda dhidi ya rais Bashar al-Assad.

Awali rais Obama alisema kuwa muungano huo wa upinzani ulioundwa mwezi mmoja uliopita, sasa unatosha kuwakilisha raia wa Syria. Lakini nusura aruhusu Marekani kutoa silaha kwa upinzani.

Muungano huo tayari umetambuliwa na Muungano wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa , Uturuki na nchi kadhaa za Kiarabu.

Aidha mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka nchi 70 wanaojiita marafiki wa Syria, wanakutana mjini Marrakesh, Morocco, hii leo kujadili mzozo unaoendelea nchini humo.

Huu ni mkutano wa nne wa wale wanaojiita marafiki wa Syria na mara hii umehudhuriwa na Muungano wa vyama vya upinzani vya Syria.

Rais Obama emetambua muungano wa vyama vya upinzani Syria kama waakilishi halali wa wananchi wa Syria

Marekani ilitangaza kuutambua muungano wa upinzani kama wawakilishi halali wa watu wa Syria.

Marafiki hao wa Syria wamemtaka rais Assad aondoke mamlakani na kumuonya dhidi ya kujaribu kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.

Mkutano huu unafanyika wakati majeshi ya Assda yakipambana vikali na waasi viungani mwa mji mkuu Damascus, ambao ndio ngome kuu ya rais Assad.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.