Uwindaji haramu tisho kwa uthabiti wa nchi

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 13:50 GMT

Pembe zilizonaswa za ndovu

Hazina ya kimataifa ya wanyamapori, inasema kuwa biashara haramu ya wanyamapori inatishia uthabiti wa baadhi ya serikali , hasa barani Afrika.

Katika ripoti yake mpya,hazina hiyo ya uhifadhi wa wanyamapori, inasema kuwa pesa kutoka kwa biashara hiyo haramu, ambayo ina thamani ya dola bilioni moja kila mwaka, zinatumiwa kufadhili mizozo ya wenyewe kwa wenyewe.

Inaongeza kuwa waasi nchini Chad, Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamenunua silaha kwa pesa zinazotokana na biashara ya pembe za ndovu pamoja na bidhaa zengine zinazotokana na wanyama hao.

Ripoti inasema kuwa biashara hiyo haramu, imeongezeka mara dufu katika mwongo mmoja uliopita.

Utafiti wa hazina hiyo unakuja wakati maafisa wa Malaysia, wamenasa tani mbili za pembe za ndovu ikiwa tukio la kwaza ambapo idadi kubwa zaidi ya pembe za ndovu imewahi kunaswa.

Makundi ya waasi barani Afrika yanapata faida kubwa kutoka kwa pembe za Ndovu, Chui wakubwa na Vifaru ili kufadhili harakati zao.

Kupiga hatua

Udhalimu unaotendewa wanyama pori na wawindaji haramu

Kabla ya hazina hiyo kutoa ripoti yake , maafisa wa uhamiaji nchini Malyasia waliripoti kunasa kiwango kikubwa zaidi kuwahi kunaswa cha pembe za Ndovu.

Kulingana na maafisa hao, pembe hizo zilikuwa zinapelekwa nchini China kutoka Togo na zilikuwa pembe 1,500

  • Mamia ya Vifaru huuwawa kila mwaka , wawindaji wakitaka pembe zao, ambazo zinaaminika kuweza kuponya baadhi ya magonjwa kama saratani.
  • Kati ya mwaka 2008 na 2011, magenge ya wahalifu, yaliwaua zaidi ya vifaru 800, kulingana na shirika moja la kuchunguza idadi ya wanyama wanaouawa kiharamu.
  • Nchini Afrika Kusini ambako kuna idadi kubwa ya Vifaru, vifaru 455 waliuawa mwezi Oktoba mwaka 2012.
  • Bei ya pembe za Vifaru ilipanda hadi dola 65,000 kwa kilo moja mwaka 2012. Mnamo mwaka 2011, zilikuwa zinauzwa, dola 35,000.

Ziligunduliwa zikiwa ndani ya kreti za mbao, ambazo zilikuwa zimefanywa kuonekana kama mbao ambazo zilikuwa tayari kutumika.

Kunaswa kwa pembe nyingi hivyo kwa wakati mmoja, ni habari njema, ambayo pia ni nadra kwa wale wanaohusika na kupambana na biashara haramu ya wanyma apori.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.