Shabiki wa kufa kupona Italia

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 07:32 GMT

Timu ya Udinese

Shabiki mmoja nchini Italy alijipatia umaarufu nchini humo kwa kuwa shabiki wa pekee kufika uwanjani wakati wa mechi ya soka ya ligi kuu ya Italia (serie A) kuunga mkono timu yake.

Arrigo Brovedani -- shabiki wa kilabu ya Udinese -- alijipata akiwa shabiki peke yake katika uwanja wa Sampdoria wenye maelfu ya viti usiku wa majira ya baridi.

Alizomewa na kukejeliwa na mashabiki wa timu ya wenyeji Sampdoria.

Lakini Arrigo alipeperusha bendera yake na kushangilia timu yake na kisha kuondoka uwanjani mshindi kwani timu yake hatimaye ilishinda mabao mawili kwa nunge huku mashabiki hasimu wakiamua kumpongeza kwa kumpeleka eneo la kujivinjari angalau kwa kinywaji.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.