Wahimizwa kula zaidi viazi Sudan

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 13:36 GMT

Msichana mdogo akiwa amebeba ndoo ya viazi akiwa na kakake mdogo nchini Sudan

Tamasha la viazi linafanyika katika mji mkuu wa Sudan , Khartoum, kwa lengo la kuwahamasisha watu kula na kulima zaidi viazi .

Maharagwe, wali , mihogo na nafaka nyingine vimekuwa vyakula vikuu zaidi kuliko viazi nchini Sudan na maeneo mengine ya Afrika

Zaidi ya vyakula sitini vilivyoandaliwa kwa viazi vitaandaliwa katika tamasha hilo kuwawezesha watu kuonja.

Kutakuwa pia na maonyesho ya mbinu za ukulima wa viazi na namna ya kuvihifadhi .

Waandalizi wa mkutano huo wanasema kuwa Sudan inaweza kuwa mzalishaji mkuu wa viazi barani Afrika kutokana na hali yake ya hewa na raslimali kubwa ya ardhi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.