Waasi wa Somalia wa Al Shabab washindwa kijeshi

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 06:39 GMT
Jeshi la AU nchini lililopo Somalia

Jeshi la AU nchini lililopo Somalia

Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, anasema kundi la wanamgambo wa Al Shabab limeshindwa kijeshi.

Bwana Mohamud ameiambia BBC kuwa serikali yake inawatuma wazee wa kimbari ili kuwashawishi vijana waliokuwa wamehadaiwa kujiunga na Al Shabab, kutupilia mbali alichosema ni maadili potovu na kusitisha ghasia.

Serikali ya Somalia imekuwa ikiimarisha utawala wake, na kudhibiti nchi hiyo ikisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika. Kabla ya sasa, Somalia ilikuwa haijawa na serikali rasmi kwa zaidi ya miaka 20.

Hassan Sheikh Mohamud alichukua hatamu za uongozi mwezi Septemba mwaka huu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.