Syria yawafyatulia waasi makombora ya 'Scud'

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 05:57 GMT
Makombora aina ya Scud

Makombora aina ya Scud

Maafisa kutoka Marekani na shirika la kujihami la NATO wanasema jeshi la Syria limekuwa likifyatua makombora ya masafa mafupi katika vita dhidi ya waasi, huku mzozo nchini humo ukizidi kuzorota.

Maafisa hao, ambao hawakutaka kutajwa, wanasema makombora hayo, yanofanana na yale ya Scud, yalifyatuliwa kutoka Damascus hadi maeneo ya kaskazini yanayodhibitiwa na waasi.

Msemaji mmoja wa Wizara ya Nchi za Kigeni wa Marekani, Victoria Nuland, alisema serikali ya Syria inatumia silaha hatari.

Ingawaje alisema kuwa hatatoa "habari za kinaganaga kuhusu makombora hayo", alithibitisha kwamba "hivi majuzi ufyatuliaji wa makombora ulikuwa umeonekana".

Upinzani

Bi Nuland alisema: "Vile serikali hiyo inavyozidi kukata tamaa ndivyo tunavyoshuhudia kuongezeka kwa visa vya ukatili na kutumika kwa silaha kali zaidi."

Msemaji wa White House Jay Carney alisema iwapo taarifa kusuhu urushaji wa Scud ni za kweli basi "hili ndilo tukio la hivi karibuni kutoka serikali inayokata tamaa, na ambayo imepuuza umuhimu wa maisha ya binadamu na wa wananchi wake".

Jumatano, zaidi ya nchi 100 chini ya jina Marafiki wa Syria, zilikutana nchini Morocco na kukubali kutambua upinzani wa National Coalition for Syrian Revolutionary and Opposition Force, kiwe chama pekee kitakachowakilisha wananchi wa Syria.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.