Afutwa kazi kwa kuvunja sheria ya ndoa China

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 14:44 GMT

Wazazi wanaruhusia tu kupata mtoto mmoja nchini China

Afisaa mmoja mkuu nchini China ameachishwa kazi kufuatia madai kuwa alivunja sheria ya ya ndoa ya nchi pamoja na sheria ya kuruhusiwa tu kuwa na mtoto mmoja.

Inaarifiwa kuwa afisaa huyo, Li Junwen alivunja sheria kwa kuwa na wake wanne na watoto kumi.

Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa bwana, Li Junwen, alipata watoto wanne na mke wake wa kwanza na tayari alikuwa ameishi na wanawake wengine watatu ambao alipata nao watoto waliosalia.

Chinese writer

Mwandishi wa China Ma Jian aliyeandika kitabu kinachoelezea mateso wanayopitia wanawake wa China chini ya sheria ya mtoto mmoja

Maafisa wanasema anachunguzwa kwa kosa hilo ingawa kusheria haileweki uhusiano aliokuwa nao na wanawake hao.

China inaruhusu tu wazazi kuwa na mtoto mmoja la sivyo walipe faini kwa serikali kila mtoto wa ziada.

Inajulikana kuwa wanawake wengi nchini China hulazimishwa kutoa kimba zao wanapojulikana kuwa na mbimba ya pili.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.