Gazeti la China Daily lazinduliwa Kenya

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 09:30 GMT

Gazeti la China Daily

Gazeti kubwa zaidi nchini Uchina, limezindua gazeti lake la kiingereza kuhusu maswala ya Afrika , ikiwa ndio uzinduzi wake wa hivi karibuni kuhusu vyombo vya habari barani Afrika.

Gazeti hilo la kila wiki na ambalo pia linakuja kwa mfumo wa dijitali, linalenga kufafanua zaidi kuhusu uhusiano wa China na Bara la Afrika.

Kituo cha televisheini cha China CCTV pamoja na shirika la habari la Xinhua zina matawi barani Afrika.

Nchi hiyo ina ushawishi mkubwa barani humo kiuchumi ikiwemo teknolojia ya mawasiliano na uwekezaji wa miundo msingi.

Gazeti hilo litakuwa likichapishwa mjini Nairobi, Kenya.

''Uhusiano kati ya China na Africa ni muihumu sana katia dunia ya leo'' alisema mhariri mkuu wa gazeti hilo. Zhu Ling.

"bado unakuwa na huwa ni uhusiano mgumu kufafanua au kueleweka. Tunatumai kutoa maelezo ya kina kuhusu uhusiano huu.''

Waziri wa habari wa Kenya Samuel Poghisio, alinukuliwa akisema kuwa gazeti hilo litatoa mwangaza zaidi kuhusu uhusiano wa China na Afrika.

Mapema mwaka huu, televisheii ya taifa China CCTV ilifungua makao makuu nchini Kenya. Xinhua na redio China Kimataifa, pia zinandelea kupanua kazi zao Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.