Maandamano kabla ya kura ya maoni Misri

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 15:35 GMT

Polisi wakishika doria mjini Alexandria

Wapinzani na wafuasi wa Rais wa Misri Mohammed Morsi kwa sasa wanafanya mikutano mikubwa kabla ya sehemu ya kwanza ya kura ya maamuzi itakayofanyika Jumamosi.

Wapiga kura wataamua kuhusu rasimu ya katiba mpya ambayo inaungwa mkono na waislamu wakijumuisha Rais Morsi. Wapinzani wanasema rasimu hiyo imeandikwa vibaya.

Wameikashifu wakisema kuwa Rais anajaribu kuipitisha rasimu hiyo bila kufanya mashauriano yanayohitajika.

Kura hiyo ya maamuzi itasimamiwa na Idara ya Mahakama lakini majajii wengi wanasema kuwa watasusia shughuli hiyo.

Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi anasisitiza kuwa katiba inastahili kukamilisha kipindi cha mpito kutoka kwa utawala wa Hosni Mubarak

Utata huu umeibua maandamano makubwa nchini Misri pamoja na ghasia kutokea ndani na nje ya mji wa Alexandria.

'Ushindi wa kiisilamu'

Maandamano ya makundi hasimu

Huku mwanzo wa kura ya rasimu hiyo ya katiba ukikaribia, hali ya usalama imedhibitiwa huku maelfu ya polisi pamoja na maafisa wengine wa usalama wakishika doria.

Rais Morsi, pia amelipa jeshi mamlaka ya kuwakamata raia huku akisababisha wasiwasi kuwa Misri inarejea katika utawala wa kidikteta.

"Nitasusia kura hii ya maoni ....Nchi hii haihitaji migawanyiko zaidi alisema mwanamke mmoja wa Misri "

Sauti za Misri: Kura ya maoni

Hali ya usalama hata hivyo haijazuia ghasia kati ya makundi hasimu katika mji wa bandarini wa Alexandria.

Mamia walipigana kwa kurushiana mawe na silaha zengine. Magari kadhaa yalichomwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa.

Ghasia zilitokea baada ya mhubiri mmoja kuwataka waumini kupigia rasimu hiyo kura ya ndio

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.