Mamake waziri aachiliwa Nigeria

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 15:04 GMT

Wapiganaji walioko katika eneo la Delta hutekeleza visa vya utekaji nyara mara kwa mara

Serikali ya Nigeria imesema kuwa mamake waziri wa fedha , Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye alikuwa ametekwa nyara kutoka nyumbani kwake katika jimbo la Delta siku tano zilzopita ameachiliwa.

Gavana wa jimbo la Delta (Emmanuel Uduaghan) ameimabia BBC kuwa Kamene Okonjo aliachiliwa bila fujo yoyote na hakuna fedha za ukombozi zilizolipwa ili aachiliwe.

Jummanne jeshi la Nigeria liliwakmata zaidio ya watu sitini katika eneo alilotekewa nyara mama okonjo.

Kwa sasa haijulikani ikiwa walitoa kikombozi kabla ya kuachiliwa kwa mamake waziri huyo.

Gavana wa jimbo hilo alisema kuwa sio sera ya serikali kulipa kikombozi ili kuachiliwa kwa mateka lakini wakati mwingine familia huzungumza na wapiganaji hao kwa faragha kuona ikiwa wanaweza kuwaachilia jamaa zao.

''Kwa upande wetu sisi hatukusema chochote kuhusu kikombozi na wala hatukukubali kulipa wala kushauriana na watekaji nyara kuhusu kuwalipa,'' alisema gavana huyo.

Mwanamume aliyemleta nyumbani Bi Okonjo kwa sasa amekamatwa na polisi na anahojiwa kuhusu yaliyojiri.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara nchini Nigeria na wala taarifa hizo huwa hazigongi vyombo vya habari.

Wafanyabiashara, wacheza soka, na wasomi wamekuwa wakitekwa nyara huku watekaji wao wakidai kikombozi katika maeneo ya Kusini katika siku za hivi karibuni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.