Wamisri wengi wapiga kura ya maoni

Imebadilishwa: 15 Disemba, 2012 - Saa 17:03 GMT

Wananchi wengi wa Misri wamejitokeza kushiriki kwenye kura ya maoni kuhusu katiba iliyogawa nchi, huku kukiwa na ulinzi mkubwa katika duru ya kwanza ya kura hiyo.

Foleni ya kupiga kura nchini Misri

Upigaji kura uliongezwa muda wa saa mbili katika majimbo kumi pamoja na Cairo na Alexandria, ambako kura inafanywa Jumamosi.

Mkuu wa jeshi aliiambia BBC kwamba ameridhika na hali ndani na nje ya vituo vya kupigia kura.

Lakini upinzani wa ushirikiano wa National Salvation Front umekilaumu chama cha Muslim Brotherhood kuwa kimefanya udanganyifu kwenye kura.

Upinzani unasema katiba iliyopendekezwa inaelemea sana upande wa Uislamu na hailindi haki za raia.

Duru ya pili ya kura ya maoni itafannywa baada ya juma moja.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.