Mkutano mkuu wa ANC waanza Afrika Kusini

Imebadilishwa: 16 Disemba, 2012 - Saa 13:38 GMT

Chama tawala cha Afrika kusini, ANC, kimeanza mkutano wake wa taifa leo mjini Mangaung ambako chama hicho kiliundwa miaka 100 iliyopita.

Wajumbe wa ANC nje ya mkutano wa chama

Katika kikao hicho chama kitachagua viongozi wake.

Nje ya ukumbi wa mkutano baadhi ya wajumbe waliimba wakati wamepanga foleni kuingia ndani.

Rais Jacob Zuma atapambana na naibu wake, Kgalema Motlanthe, kuania uongozi.

Waandishi wa habari wanasema mkutano huo unafanywa wakati ANC inajitetea kupata imani ya wafuasi, huku chama kikizungukwa na tuhuma za rushwa kutoka serikali za mitaa hadi ofisi ya rais.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.