Mauaji haya ni sharti yakome-Obama

Imebadilishwa: 17 Disemba, 2012 - Saa 12:31 GMT
Rais Obama

Rais Obama akiwahutubia waumini wa madhehebu mbali mbali

Rais wa marekani Barack Obama ameahidi kutumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa mkasa wa ufyatuliaji risasi kama ule uliotokea katika mji wa Newtown, jimbo la Connecticut, ambapo mtu aliyejihami kwa bunduki aliwauwa watu 26 wakiwemo watoto ishirini wa shule ya msingi hautokei tena.

Akiwahutubia waumini wa madhehebu mbali mbali waliokesha kuwaenzi waliouwawa, bwana Obama alisema ili kuepuka mikasa kama hiyo, Marekani ni sharti ibadilike.

Bofya Rais Obama aliwaambia wakaazi wa eneo hilo kuwa taifa la Marekani linaomboleza.

Watoto 20 na wanawake 6 waliuawa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa katika shule ya Sandy Hook, na mtu mmoja ambaye pia alijiua kwa kujipiga risasi.

Rais Obama kushinikza sheria mpya

Raia Connecticut

Raia Connecticut wakiomboleza

Mazishi wa watoto wawili waliouawa kwenye tukio hilo yamefanyika hii leo.

Polisi wanasema mtu huyo aliyekuwa amejihami kwa bunduki na Adam Lanza mwenye umri wa miaka 20.

Mtu huyo alimuua mamake kwa kumpiga risasi kabla ya kuelekea shuleni anakofunza akiwa na gari lake.

Polisi wanasema mshukiwa huyo alikuwa na mamia ya risasi na alitumia bastola ya rashasha kama silaha yake maalum.

Mshukiwa huyo pia alikuwa amebeba bunduki zingine mbili ambazo zilipatikana ndani ya gari lake.

Kwa mara nyingine tena rais Obama alikariri haja ya kuchukua hatua dhidi ya uhalifu unaotekelezwa kwa kutumia bunduki, na kusema kuwa katika siku za hivi karibuni, atatumia kila mbinu na madaraka aliyo nayo kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halitatokea tena.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.