Rais wa Tunisia arushiwa mawe na nyanya

Imebadilishwa: 17 Disemba, 2012 - Saa 19:16 GMT

Maandamano ya umma Tunisia

Waandamanaji mjini Sidi Bouzid wamemrushia rais wa Tunisia, Moncef Marzouki nyanya na mawe.

Walinzi wa riasi huyo Tunisia, taifa ambalo mageuzi katika nchi za Kiarabu yalianziawalimuondoa kutoka mahala hapo na kukatiza mkutano wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwake.

Mchuuzi mmoja Mohamed Bouazizi, alijiteketeza moto mjini Sidi Bouzid, na kupelekea maandamano makubwa yaliyosaababisha kuondolewa madarakani kwa serikali iliyopita.

Serikali ya sasa imekabiliwa na maandamano kutoka kwa raia ambao wanahisi kuwa serikali ya sasa haifanyi lolote kuimarisha hali ya maisha yao.

Waandamanaji hao walivamia eneo ambalo rais Marzouki, alikuwa amelihutubia umati wa watu wapatao elfu tano.

Raia wataka serikali kuimarisha hali ya maisha

Moncef Marzouki

Rais wa Tunisia Moncef Marzouki

Raia hao waliojawa na hasira walirusha mawe na nyanya na kulazimisha walinzi wa rais kumuondoa kutoka mahala hapo pamoja na spika wa buneg Mustapha Ben Jaafar.

Waandamanaji hao waliimba nyimbo zinazosema ''raia wanataka kuanguka na serikali'', moja ya kauli mbiu iliyotumiwa kuangusha serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Zine al-Abidine Ben Ali, Januari 2011.

Machafuko hayo kisha yakasambaa hadi Misri, Libya na mataifa mengine ya Kiarabu.

Katika hotuba yake, rais Marzouki alihaidi mageuzi ya kiuchumi katika kipindi cha miezi sita ijayo kwa raia hao wa Sidi Bouzidi, moja ya miji masikini zaidi nchini humo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.