Wakimbizi waamriwa kurudu kambini Kenya

Imebadilishwa: 18 Disemba, 2012 - Saa 11:31 GMT
Shambulio la Kigaidi mjini Nairobi

Raia wakijaribu kuwaokoa watu kufuatia shambulio la kigaidi mjini Nairobi

Wakimbizi wote wenye asili ya Kisomali nchini Kenya, wameamriwa kuondoka katika maeneo ya mijini na kurudi kambini baada kuwepo kwa milipuko ya mara kwa mara.

Misaada haitatolewa tena kwa yeyote ambaye atakuwa mjini, amesema mkuu wa shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa.

Milipuko hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu wenye asili ya Kisomali, kama vile mkoa wa Kaskazini Mashariki na mtaa wa Eastleigh iliyoko mjini Nairobi.

Mashambulizi hayo yanaaminika kufanywa na watu wanaoaminika kuwa wanachama cha kundi la Kiislamu la Al Shabab.

Maelezo zaidi hivi punde

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.