Watu 4 wauawa na wanamgambo Pakistan

Imebadilishwa: 18 Disemba, 2012 - Saa 11:01 GMT
Watoto nchini Pakistan

Watoto nchini Pakistan wakipanga foleni kupew chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza

Watu waliojihami kwa bunduki wamewauwa kwa kuwapiga risasi wanawake wanne waliokuwa wakitoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza au polio nchini Pakistan.

Mashambulizi hayo yametokea katika maeneo matatu tofauti ya mji mkuu wa taifa hilo Karachi, ambako maafisa wamesema sasa kampeni ya kutoa chanjo hiyo imesimamishwa.

Haijabainika ni nani aliyewauwa wanawake hao lakini viongozi wa Taliban awali walikuwa wamesema kuwa kampeni hiyo ni kisingizio cha kufanya ujasusi na njama ya kuwapokonya Waislamu uwezo wa kuzaana.

Ugonjwa wa polio umezagaa nchini Pakistan na shirika la afya duniani WHO, lilikuwa limezindua kampeni ya kutoa chanjo kwa watoto nchini humo mapema wiki hii.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.