Ripoti ya shambulio la Benghazi imetolewa

Imebadilishwa: 19 Disemba, 2012 - Saa 10:16 GMT
Ubalozi wa Marekani mjini Benghazi

Ubalozi wa Marekani mjini Benghazi, baada ya kushambuliwa

Ripoti kuhusu shambulizi dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Bengazi, mwezi Septemba imekosoa mpangilio wa kiusalama iliyowekwa katika ubalozi huo na kuitaja kama isoyokamilika.

Balozi wa marekani nchini Libya, pamoja na Wamarekani wengine watatu waliuwawa kufuatia shambulizi la wanamgambo dhidi ya ubalozi huo.

Kuuawa kwa balozi Christopher Stevens na raia wengine watatu kulizua lawama za kisiasa mjini Washington kwa kipindi cha miezi mitatu.

Tume huru iliyoteuliwa kuchunguza kisa hicho imesema kuwa ubalozi huo mdogo mjini Bengazi, haukupewa ulinzi wa kutosha licha ya maafisa kutoa ombi la mara kwa mara waongezewe walinzi zaidi.

Ripoti hiyo inasema hatua ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni kutegemea wanamgambo kutoa ulinzi kwa ubalozi huo haikuwa nzuri.

Kuvunjika kwa mawasiliano katika idara mbili za wizara hiyo kulimaanisha kuwa ubalozi huo haungeweza kujilinda.

Ripoti hiyo inapendekeza pesa zinazotengewa shughuli za ulinzi katika balozi za nje iongezwe na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Hillary Clinton, ameamuru matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mapendekezo kutekelezwa mara moja na kikamilifu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.