Waasi watishi mapinduzi Chad

Imebadilishwa: 19 Disemba, 2012 - Saa 11:12 GMT
Ramani ya Chad

Ramani ya Chad

Chad imetuma wanajeshi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati ili wapambane na waasi walioteka eneo la Bria, lenye utajiri mkubwa wa madini ya almasi.

Rais wa nchi hiyo Francois Bozize, ameripotiwa akiomba msaada wa kijeshi kutoka nchi jirani baada ya majeshi yake kushindwa kukabiliana na waasi hao.

Umoja huo wa waasi unamlaumu rais Bozize kwa kushindwa kufuata baadhi ya vipengele vilivyowekwa kwenye makubaliano ya amani ya mwaka 2007.

Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ikikabiliwa na mfululizo wa mapinduzi yanayofanywa na waasi tangu nchin hiyo ilipojinyakulia uhuru wake mwaka 1960.

Kufuatia mashambulizi hayo, Chad mara nyingi imejikuta ikiingilia kati.

Chad imemsaidia rais Bozize pindi alipochukua madaraka miaka tisa iliyopita, na pia ilimsaidia mwaka 2010 pindi alipokuwa akipambana na makundi ya waasi.

Kundi la waasi la Seleka, ni mjumuiko wa makundi matatu ya wanajeshi, ambao wanamlaumu rais kwa kushindwa kutimiza masharti ya kusitisha mashambulizi na mpango wa kuawaachilia huru wafungwa wa kisiasa na kulipwa kwa wapiganaji ambao watasitisha mapigano na kujiunga na upande wa serikali.

Umoja huo wa waasi umetishia kupindua serikali iwapo rais Bozize atashindwa kufanya majadiliano.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.