Hollande akiri Ufaransa ilitekeleza uovu

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 11:14 GMT
Francois Hollande

Rais wa Ufaransa Francois Hollande

Rais wa Ufaransa Francois Hollande, amekiri ukatili uliotekelezwa na taifa lake wake wakati ilipokuwa ikitawala Algeria wakati wa ukoloni, lakini hakuomba msamaha.

Akiongea kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yake nchini Algeria, kama rais wa Ufaransa, rais Hollande, aliliambia bunge na nchi hiyo kuwa ''anatambua mateso na dhuluma ambazo zilisababisha na ukoloni dhidi ya raia wa Algeria''.

Lakini rais huyo wa Ufaransa, aliongeza kuwa hakuja nchini humo kuomba msamaha.

Maelfu ya raia wa Algeria, waliuawa wakati wa vita vya uhuru wa taifa hilo vilivyodumu kwa muda wa miaka saba.

Je rais wa Ufaransa ataomba msamaha?

Rais wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa akiwa na mwenzake wa Ufaransa

Jeshi la Ufaransa, limeshutumiwa kwa kutekeleza mauaji ya raia na kutumia mateso wakati ilipokuwa ikijaribu kuzima uasi dhidi ya serikali kutoka kwa wanaharakati wa uhuru.

Hata hivyo raia wengi wa Ufaransa, pia waliuawa wakati wa vita hivyo baada ya raia wa Alheria kuwashambulia kulipisa kisasi kabla ya Algeria, kupata uhuru wake mwaka wa 1962.

Rais Hollande, amesema kunahaja ya kusema ukweli na kutambua kuwa haki za raia wa nchi hiyo zilikiukwa.

Amesema Ziara yake imefungua awamu mpya ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ambazo ni sawa.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Algeria, miaka mitano iliyopita, mtangulizi wa rais Hollande, Rais Nicolas Sarkozy, pia alikiri kuwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa wa miaka 132 ulisababisha maafa na dhuluma nyingi dhidi ya raia.

Sawa na rais Hollande rais Sarkozy hakuomba msamaha.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.