LRA yatuhumiwa na uwindaji haramu

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 18:05 GMT
Joseph Kony

Joseph Kony kiongozi wa LRA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limeagiza uchunguzi kufuatia ripoti kuwa waasi wa Lords Resistance Army LRA, wanawinda ndovu na kuuza pembe zao.

Kundi hilo na kiongozi wake kutoka Uganda, Joseph Kony, wanatuhumiwa kutumia fedha wanazopata kutoka kwa mauzo ya pembe za ndovu kufadhili machafuko katika mataifa manne ya Afrika,Uganda, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.

Ndovu hizo zinasemekana kuwindwa nchini Congo.

Daktari Iain Douglas Hamilton, ni mwanzilishi wa shirika la Save the Elephants ameiambia BBC kuwa idadi ya ndovu barani afrika inaendelea kushuka kutokana na uwindaji haramu hasa katika mataifa hayo manne.

Amesema ukosefu wa usalama na vyombo vya serikali katika maeneo husika yamechangia pakubwa kuongezeka kwa visa vya uwindaji haramu barani Afrika.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuimarisha msako wao dhidi ya kiongozi wa kundi hilo la LRA, Joseph Kony. Kony anasakwa na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kuhusiana na uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadamu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.