Raia wa Ufaransa atekwa nyara Nigeria

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 10:52 GMT
Habari za hivi punde

Habari za hivi punde

Kundi la watu wapataoo 30 waliokuwa wamejihami kwa bunduki wametumia baruti kushambuliwa jengo moja lenye ulinzi mkali, Kaskazini mwa Nigeria, na kumteka nyara mhandisi mmoja raia wa Ufaransa.

Idara ya polisi nchini Nigeria imethibitisha tukio hilo na kusema kuwa watu wawili waliuawa katika shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Katsina.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Abdullahi Magaji, amesema kundi hilo kisha likavamia kituo kimoja cha polisi, ili kuzuia maafisa wa polisi kuwafuata

Jimbo la Katsina limekuwa tulivu na halijaathirika na machafuko yanayoendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Nigeria yanayosababishwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.