Mancini kumsamehea Balotelli

Imebadilishwa: 21 Disemba, 2012 - Saa 12:24 GMT
Mario Balotelli

Mario Balotelli akipewa kadi nyekundu

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini, amesema yuko tayari kuumpa mshambulizi wake Mario Balotelli nafasi nyingine, ikiwa ataonyesha kuwa anahitaji.

Mapema wiki hii Balotelli, alifutilia mbali uamuzi wake wa kukataa rufaa dhidi ya uamuzi wa klabu hiyo wa kumpiga faini ya mshahara wake wa wiki mbili, kwa kukosa mechi kumi na moja msimu uliopita.

Wakati alipoulizwa ikiwa Balotelli, atapewa nafasi nyingine, Mancini alisema ''Hakika, Mimi kama kocha wake na kama wachezaji wengine, ikiwa atastahili nafasi nyingine, sitakuwa na buda ila kuumpa nafasi hiyo. Lakini ni jukumu la Balotelli kudhihirisha kuwa anahitaji nafasi hiyo''

Balotelli, mwmenye umri wa 22, atakosa mechi ya kesho dhidi ya Reading kwa kuwa ni mgonjwa.

Maelezo zaidi baadaye

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.